القدر

Al-Qadr

Sura ya 97 · ya Makka · aya 5 · Mpangilio wa kuteremshwa: 25

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLaylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHuteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.