البينة
Al-Bayyinah
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,
- Ali Muhsin Al-BarwaniYaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdani yake mna maandiko yaliyo nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika walio amini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMalipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao waradhi naye. Hayo ni kwa anaye mwogopa Mola wake Mlezi.